October 24, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chadema: Tushajua alipo Heche, polisi waujulishe umma

 

JOHN Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amesema kuwa amedokezwa na mmoja wa maofisa wa Jeshi la Polisi kuwa John Heche, Makamu mwenyekiti wa Chama hicho yupo Dodoma. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Jana tumepata uhakika kwamba yupo Dodoma, amefikiwa na mmoja wa wanafamilia …Leo nimepata taarifa kwamba mchana huu ofisa wa idara ya uhamiaji amefika pale kituo cha polisi cha Dodoma kwa ajili ya kumhoji Makamu Mwenyekiti wetu ”

Mnyika, ametoa wito kwa jeshi la Polisi kutoa taarifa kwa umma alio Heche, na hali yake “hivi ni visingizio vya kutaka kuendelea kumshikiri kuelekea tareje 29 na baada ya tarehe 29 Oktoba”.

About The Author

error: Content is protected !!