SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC), limetangaza kusitisha safari, hadi kutakapotolewa taarifa mpya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kusitishwa kwa safari hizo, kumefuatia treni ya Electric Multiple Unit – EMU, maarufu treni ya mchongoko, kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani.
Treni hiyo, ilikuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea Dodoma, leo Alhamisi 23 Oktoba 2025.
Afisa mmoja kutoka Idara ya Uhusiano ya TRC, ameliambia gazeti hili, bado wanasubiri mafundi ili waweze kutoa taarifa mpya.
“Tunasubiri mafundi ili waseme tatizo hili limetokana na nini na limesababisha hasara kwa kiasi gani,” ameeleza.
Ameongeza, “…hakuna treni iliyoruhusiwa kuanza safari mpaka pale mafundi watakapotoa taarifa mpya. Muda rasmi wa kuanza safari hatujajua maana mafundi bado hawajatoa taarifa yoyote mpya.”
Mapema asubuhi, TRC ilitaja chanzo cha ajali hiyo kutokana na “hitilafu za kiuendeshaji.”
ZINAZOFANANA
Machafuko ya 29 Oktoba: Maaskofu Katoliki wataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wawajibike
Halloween yaja na mchezo mpya wa kusisimua, Trick or Treat Bonanza ya Meridianbet
Shinikizo la kufanyika uchunguzi wa mauaji ya 29 Oktoba lashika kasi