October 11, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mgombea udiwani Kinyerezi ajinadi kuwa mtu wa vitendo zaidi

 

MGOMBEA Udiwani wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Kinyerezi wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, John Mrema Ryoba amewahakikishia wapiga kura wa Kinyerezi kwamba yeye si mtu wa maneno katika kuhakikisha anaibadilisha Kinyerezi kimaendeleo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Mrema aliyasema hayo leo katika mkutano wa mashabiki wa klabu ya mpira ya Simba uliofanyika katika viunga vya Kinyerezi Park.

Akizungumzia mustakabali wa michezo alisema: “Ndugu zangu nawaomba kata yetu ilikwama kwa muda mrefu sasa chama kimeleta mgombea mwingine tunazo shughuli nyingi za kufanya ikiwemo kushughulikia suala la takataka, barabara mbovu, michezo hakuna amshaamsha ya michezo kama Kata nyingine , nina waomba wana Simba tusiwe nyuma kwenda kupiga ifikapo Oktoba 29.”

Kwa mujibu wa Mrema; “Mwenyekiti wetu wa chama taifa ambaye ndiye mgombea mgombea wetu kwa nafasi ya Urais ametuhakilosha hali ya usalama kuimarishwa.”

Mrema alifafanua hilo kutokana na swali aliloulizwa na mmoja wa mashabiki wa Simba, Rachel Steven kuhusu ya usalama siku ya kupiga kura; “Niwahakikishie Mwenyekiti wetu ambaye ni mgombea ametuthibitishia vyombo vya usalama vimejipanga tunakwenda kufanya Uchaguzi wa amani.

Mrema alisema, “Mimi ninawaomba wana Simba bonanza litafanyika baada ya uchaguzi, nimekuwa mdau wa michezo hata kabla ya kiwanja nafasi hii. Mimi sio mtu wa kuahidi, mimi ni mtu wa kutenda. Naomba mridhike mmepata kiongozi nataka Kinyerezi iwe Kata ya mfano katika kata zote za ndani ya Jimbo la Segerea.”

About The Author

error: Content is protected !!