October 9, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kitabu cha Lissu chazua gumzo mahakamani

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

KITABU cha Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, kinachohusu uchaguzi na mifumo yake nchini Tanzania kimezua gumzo katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam anakoshtakiwa kwa kosa la uhaini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kesi hiyo Na. 19605/2025 inasikilizwa mahakamani hapo na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Jaji Dunstan Ndunguru, akishirikiana na Jaji James Karayemaha na Jaji Ferdinand Kiwonde ambapo leo tarehe 9 Oktoba 2025, upande wa Jamhuri uliwasilisha mahakamani hapo shahidi wa pili ofisa wa polisi Insepekta John Kaaya (45) ambaye anafanya kazi kwenye dawati la doria ya mtandaoni ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wakati Jaji Ndunguru anakwenda kuahirisha shauri hilo ili kesho Lissu alipata nafasi ya kumuuliza maswali ya dodoso shahidi huyo Lissu aliwaeleza majaji hao kuwa angependa wasome kitabu chake cha “Remaining in the Shadow” kuhusu mambo ya Uchaguzi.”

Nimebeba copy tatu (nakala tatu) hapa naomba niwape na Mawakili wa Serikali nakala moja nao wakasome ili wajue mambo mengi wasidhani mimi ni mtu wa mchezo mchezo na waache kutumika tu.

Majaji pia nawapatieni nakala moja.

Jaji Ndunguru: Sasa unatupatia copy moja tunasomaje si bora ungetoa copy mbili?

Lissu: Waheshimiwa majaji nikiwapa mbili mtagombana sana maana mko watatu.

Jaji Ndunguru: Sasa wewe ugomvi wetu haukuhusu, tupe hizo copy mbili sisi tutajua cha kufanya.

Lissu: Basi nyie Vijana anawanyooshea Wakili Paul Kisabo na Deodatus Mahinyila kuwa hakikisheni kesho mnaongeza copy zingine 4 zije hapa.

About The Author

error: Content is protected !!