Tundu Lissu akiwa mahakamani
TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo tarehe 10 Oktoba 2025, ameieleza Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam, kuwa bado idara ya uhamiaji nchini imewazuia wageni wake waliotoka nje ya nchi kwa ajili ya kusikiliza shauri la uhaini linalomkabili mahakamani mpaka wapate kibali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
“Lissu wale wageni wangu wameambiwa hawawezi kuingia ndani ya Mahakama hii hadi wapate kibali cha idara ya Uhamiaji Sasa wataendelea kuwepo hadi watakapofukuzwa kuwepo nchini hadi kibali chao cha kuwepo Tanzania kitakapoisha,”alidai Lissu kabla shauri hilo Na. 19605/2025 halijaanza kusikilizwa ambapo leo ilikuwa zamu ya Lissu kumuuliza shahidi wa pili wa serikali maswali ya dodoso.
Wakati huo huo Jaji Dunstan Ndunguru, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa anayeshirikiana na Jaji James Karayemaha, na Jaji Ferdinand Kiwonde, amesema kuwa mahakama hiyo ilishatoa utaratibu wa namna ya watu kuingia mahakamani hapo.
“Kwa hiyo tumeambiwa jambo hilo linashughulikiwa na ofisi ya msajili naomba ndugu zako wawasiliane na Ofisi ya Msajili ili wakalimalize,” amesema Jaji Ndunguru.
ZINAZOFANANA
Mwanajeshi wa Marekani akamatwa na mabomu Tanzania
Machafuko ya 29 Oktoba: Maaskofu Katoliki wataka wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wawajibike
Shinikizo la kufanyika uchunguzi wa mauaji ya 29 Oktoba lashika kasi