
TUNDU Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo tarehe 8 Oktoba 2025, ameelea kumuuliza shahidi wa kwanza wa Jamhuri kwenye kesi Na. . 19605/2025 la uhaini linalomkabili mahakamani hapo ambapo amemtaka shahidi huo kutoa tafrisi ya uasi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Fuatilia dodoso la maswali ya Lissu kwa Shahidi huyo wa kwanza wa Jamhuri ASP George Bagyemu – Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam aliyeanza kutoa ushahidi wake juzi tarehe 6 Oktoba, kama ifuatavyo :-
Lissu: Sasa tuzungumze kuhusiana na uhaini.
Ulisema kwamba nilielekeza uchunguzi wa uhaini kwasababu Lissu alisema atahamasisha uasi?
Bagyemu: Ni kweli kabisa.
Lissu: Sasa kuna mahali kokote umetafsiri neno uasi?
Bagyemu: Kuzuia uchaguzi, vitisho kwa serikali basi sikusema neno moja moja. kwahiyo sikutoa tafsiri ya neno uasi.
Lissu: Je katika hati ya mashtaka ninayoshtakiwa nayo kuna ufafanuzi wa neno tutahamasisha uasi?
Bagyemu: Huo ufafanuzi upo.
Lissu: Sasa tuambie upo wapi, Hapo kwenye hati ya mashitaka, nakusomea hati ya mashitaka ilivyosema Neno uasi limetajwa mara mbili. Je kuna mahali kokote imeandikwa?
Bagyemu: Uasi ilitafsiriwa.
Lissu: Una akili timamu wewe afisa wa polisi?
Bagyemu: Nina akili timamu ndio maana ni afisa wa Polisi.
Lissu: unaweza kuwa afisa wa polisi nchi hii na ukawa huna akili timamu.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI Digital
ZINAZOFANANA
Mauaji ya Kibiti yaibuliwa kwenye kesi ya Lissu
Lissu ambana kwa maswali shahidi wa Serikali
Kutekwa Polepole, Mawakili wake wamshtaki IGP, AG, DPP, ZPC