
SAKATA la mauaji ya Kibiti, wilaya ya Rufiji yaliyotokea 2017, limeibuliwa leo taehe 8 Oktoba 2025, kwenye shauri Na. 19605/2025 la uhaini linalomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwenye Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu akimuuliza maswali ya dodoso (Cross Examination), shahidi wa kwanza wa Jamhuri ASP George Bagyemu, Naibu Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam aliyeanza kutoa ushahidi wake juzi tarehe 6 Oktoba .
Lissu alimuuliza Bagymu idadi ya watu waliofariki kwenye mauaji ya Kibiti ikiwa yeye Naibu Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Rufiji.
Lissu: Shahidi kuna mambo nataka tumalize haraka haraka katika maelezo yako ya juzi ulisema ulishika madaraka pia ndani ya hii miaka yako 22 ya upolisi ulikuwa Deputy RCO wa Rufiji 2008.
Bagyemu: Ni kweli kabisa.
Lissu: Ulikuwa Rufiji lini?
Bagyemu: Nilikuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2018 hadi tarehe. 17 Julai 2019.
Lissu: Waeleze majaji kama Rufiji ni mkoa wa kipolisi au wilaya ya kipolisi?
Bagyemu: Rufiji ni Mkoa wa kipolisi wenye wilaya nne.
Lissu: Ni nani alikuwa RPC wako?
Bagyemu: SACP Onesmo Lyanga.
Lissu: Nani alikuwa RCO?
Bagyemu: Alikuwa anaitwa ACP Faustine Mafwele na mwingine SSP Richard Mchomvu.
Lissu: Mafwele huyu huyu?
Bagyemu: Kimya
Lissu: Nilikwambia jana uwe unajibu maswali yangu usiwe na kiherehere.
Lissu: Je kipindi kile ukiwa Deputy RCO mkuranga, kibiti, kulikuwa na mauaji mengi?
Bagyemu: Ni kipindi hicho hicho kweli nilikuwa Deputy RCO.
Lissu: Je unakumbuka idadi ya waliouawa?
Bagyemu: Sikumbuki idadi yao.
Lissu: Je unaweza kueleza sababu ya mauaji hayo mengi?
Bagyemu: Kulikuwa na makosa mengi ya kigaidi ndo maana yalikuwepo.
Lissu: Na wewe ulikuwa Deputy RCO na hujui idadi ya watu wengi waliokufa?
Bagyemu: Ungenipa muda ningekuja na idadi hiyo halisi.
Lissu: Wakati unaoneshwa ile video ulikuwa na police notebook?
Bagyemu: Yes nilikuwa nayo na hiyo notebook niliitumia kurekodi yale muhimu.
Lissu: Naomba ueleze kama uliwasilisha hiyo Police notebook?
Bagyemu: Sikuiwasilisha.
Lissu: Ulizungumza kwa kiasi kidogo juu ya mashahidi waliopatiwa ulinzi wa mahakama?
Bagyemu: Ndio ni sahihi.
Lissu: Waeleze majaji kama ulihusika kuwahoji hao mashahidi wa siri?
Bagyemu: Sikuhusika kabisa kuwahoji.
Lissu: Ieleze mahakama kama unawafahamu hao mashahidi wa siri?
Bagyemu: Siwafahamu kwa majina.
Lissu: Waeleze majaji kama uliona maombi yaliyopelekwa mahakama kuu kuwaombea ulinzi?
Bagyemu: Sikuyaona kabisa.
Lissu: Uliona hati ya viapo ya Amini Mahamba na Mossie Kahima?
Bagyemu: Sikuona kabisa.
Lissu: Je, unajua chochote kuhusu kilichofanya katika jambo hilo la mashahidi wa siri?
Bagyemu: Mimi ninachojua waliopatiwa ulinzi huo ni raia tu.
Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online, MwanaHALISI TV, na Kwenye mitandao ya kijamii MwanaHALISI Digital
ZINAZOFANANA
Update kesi uhaini: Lissu ambana shahidi tafsiri ya neno uasi
Lissu ambana kwa maswali shahidi wa Serikali
Yanayojiri kwenye kesi ya Lissu leo tarehe 7 Oktoba 2025, Mahakama Kuu