September 6, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Rais Samia kuinua sekta ya viwanda na biashara

Rais Samia Suluhu Hassan

 

MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi, Samia Suluhu Hassan ameahidi kuinua zaidi sekta ya viwanda na biashara Tanzania, kwenye ukuaji wa viwanda, amesema idadi ya viwanda vikubwa Mkoani Njombe vimeongezeka kutoka 8 hadi 17 na amesisitiza kuwa kongani za viwanda zitaanzishwa katika kila wilaya ili kuongeza ajira kwa vijana. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumzia kilimo alisema upatikanaji wa mbolea na ruzuku umeimarika,ambapo ruzuku imeongezeka kutoka tani 57,950 mwaka 2020 hadi tani 97,220 hadi 136,526.Aliwasihi vijana kujiandikisha kwa wingi ili kupata vocha za ruzuku.

Aidha ,aliahidi kuongeza uwekezaji katika chai na parachichi.Alisema serikali imechukua hatua ya kufufua viwanda vya chai ikiwemo kiwanda cha Lukondo ambacho kitawekewa mashine mpya za kusindika chai aina ya orthodox na kuanzisha vituo 50 vya kuhifadhia parachichi na mbogamboga kwa miezi mitatu ili wakulima wauze kwa bei nzuri.

About The Author

error: Content is protected !!