
Janeth Rithe
LEO tarehe 23 Juni 2025, Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama cha ACT-Wazalendo, Janeth Rithe amepewa dhamana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Rithe aliyekuwa anashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi cha Kati ameachiwa kwa sharti kwamba aripoti tena Polisi siku ya Jumatano tarehe 25 Juni 2025.
Rithe aliyejisalimisha mikononi mwa Jeshi hilo tarehe 20 Juni 2025, na kuhojiwa.
Si jeshi la Polisi au ACT waliosema Rithe alihojiwa kwa kosa gani.
Tarehe 18 Juni 2025, akiwa viwanja vya Bakharesa-Manzese jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho alionesha kushangazwa na kauli ya Rais Samia kuhusu hali ya uchumi wa Marekani.
ZINAZOFANANA
Rostam: Sekta binafsi iko tayari kuisadia ukuaji wa uchumi wa dola trilioni moja
Mohamed Abdulrahman: Gwiji la utangazaji DW laanguka
Kwaheri Joshua Nassari, Karibu DC Lawuo