
Janeth Rithe
SHANGWE Ayo, Naibu Katibu wa Uenezi wa Chama cha ACT Wazalendo, amesema kuwa chama hicho hakijajua muafaka wa Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama hicho, Janeth Rithe anayeshikiliwa tangu jana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Shangwe akizungumza na MwanaHALISI Online amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea kumshukilia Rithe bila kumpa dhamana tangu alipojisalimisha Polisi jana tarehe 20 Juni 2025.
Inadaiwa Rithe amehojiwa kwa kauli yake aliyoitoa tarehe 18 Juni 2025 kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Manzese, jijini Dar es Salaam ambapo alishangazwa na kauli ya Rais Samia ya kuhusu hali ya uchumi wa Marekani.
ZINAZOFANANA
Rostam: Sekta binafsi iko tayari kuisadia ukuaji wa uchumi wa dola trilioni moja
Mohamed Abdulrahman: Gwiji la utangazaji DW laanguka
Kwaheri Joshua Nassari, Karibu DC Lawuo