June 21, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

ACT Wazalendo: Deni la Taifa linakuwa kwa kasi, uchumi wa nchi hatarini

Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita

 

CHAMA cha ACT Wazalendo imeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la deni la taifa, ambalo hadi Aprili 2025 limefikia Sh. 107.7 trilioni kutoka trilioni 91.7 mwaka uliopita — ongezeko la trilioni 16 (asilimia 17.23). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akiwa Makao Makuu ya chama hicho, Waziri Mkuu Kivuli wa ACT Wazalendo, Isihaka Mchinjita, amesema:
“Mwenendo huu wa deni unatufikisha kwenye mstari mwekundu wa hatari ya kutokopesheka. Serikali ya CCM inatufanya tuendeshe uchumi kwa mikopo, hali inayowabebesha wananchi mzigo wa kodi na maisha magumu.”

Amesema tangu Rais Samia aingie madarakani, deni limeongezeka kwa trilioni 52.73. Aidha, kati ya trilioni 40.46 zinazokusanywa na Serikali mwaka huu, trilioni 14.2 zitaenda kulipa deni badala ya huduma kwa wananchi.

ACT imetoa mapendekezo ya kuongeza mauzo ya bidhaa nje, kupunguza uagizaji, na kurekebisha sheria za kodi kwa kampuni kubwa ili kulinda thamani ya shilingi.

Chama hicho pia kimetaja ubadhirifu wa trilioni 2.56 kwenye ripoti ya CAG na kuituhumu Serikali kwa kukosa uwajibikaji wa fedha za umma.

Leo Juni 21, 2025 Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea na desturi yake yake ya kufanya Uchambuzi wa Bajeti Kuu ya Serikali, ambapo katika awamu hii ya sita hii ndio bajeti ya mwisho kabla ya nchi haijaingia kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba.

About The Author

error: Content is protected !!