May 7, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

DC James ahamasisha wananchi kujiakindisha, kuboresha taarifa zao

 MKUU wa wilaya ya Iringa, Kheri James amewahimiza wananchi wilayani humo kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la mpiga kula kwa awamu ya pili ili kuwa na sifa za kushiriki katika uchaguzi Mkuu. Anaripoti Joyce Ndeki, Iringa … ( endelea).                                

Kheri James ametoa ujumbe huo katika ziara yake ya kuhamasisha wananchi katika mitaa na vijiji mbalimbali wilayani humo, lengo likiwa ni kuhakikisha kila Mwananchi anapata taarifa kwa wakati na anaitumia fursa hiyo kujiandikisha na kuboresha taarifa zake ili kupata uhalali wa kuchagua na kuchaguliwa.                 

Aidha amewaeleza wananchi kuzingatia maelekezo ya Tume ya uchaguzi ili kila mwenye haki ya kuandikishwa asiikose.

Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura mkoani Iringa limeanza tarehe 2 Mei 2025 na linatarajiwa kukamilika tarehe 7 Mei 2025, walengwa wakiwa ni wananchi wote ambao niwapiga kura wa mara ya kwanza, watu walio hama maeneo, watu waliopoteza kadi zao na wengine wenye sifa zilizo tamkwa na Tume.                        

Pamoja na mambo mengine Mkuu wa wilaya amewapongeza wananchi kwa kutumia fursa hiyo vizuri na amewapongeza wadau wote wa uchaguzi kwa kuendelea kuwahasisha wananchi.

About The Author

error: Content is protected !!