May 17, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Samia amteua Twange kuwa bosi Tanesco, ahamisha ma-DC wanne

 

DK. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewahamisha wakuu wa Wilaya na kumteua Jacob Twange kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco). Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 6 Mei 2025, na kitengo cha mawasiliano ya Ikulu.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais Samia amemhamisha Wakili Albert Msando kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni na kuwa Mkuu wa wilaya ya Ubungo.

Rais samia amemhamisha Japhari Kubecha kutoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni huku Dadi Kolimba akitoka Wilaya ya Karatu na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.

Wakati huo huo Lameck Nganga aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu amechaguliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo huku Bahati Mfungo akiteuluwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu ambapo kabla alikuwa Afisa tarafa ya Mbugani wilayani Arumeru.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Andrew Massawe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), akichukua nafasi ya Jaji Chande Othman aliyemaliza muda wake.

About The Author

error: Content is protected !!