March 12, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dawasa kufunga dira 65,000 za lipa kabla ya matumizi Dar

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama Bwire

 

MAMLAKA ya Maji Safi na Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imesema kuwa ufungaji wa dira za aina ya lipa kabla ya matumizi zitasaidia kwa kiasi kikubwa cha malimbikozo ya mademi kwa wateja wa majumbani na taasisi za Umma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire, alipokuwa akitoa taarifa waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Mhandisi Bwire amesema kuwa Mamlaka hiyo kwa sasa inatarajia kufunga Dira 65,000 katika Jiji la Dar es Salaam na kwa kufunga dira hizo zitapunguza malimbikizo ya madeni kwa wateja au malalamiko ya kubambikiwa bili.

Akiendelea kutoa maelezo ya mafanikio Mhandisi Bwire ameeleza kuwa kutokana na kuwepo kwa dira hizo za lipa kabla ya kutumia zitawafanya wateja wengi kutumia maji yao kadri ya mahitaji kama ilivyo kwa Shirika la Umeme nchini Tanesco.

Kiongozi huyo pia amesema kuwa katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka 4 DAWASA imepokea kiasi cha Sh. 1.2 tirioni kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Aidha amesema kuwa serikali imetoa kiasi cha Sh. 16 bilioni kwa ajili ya kubadilisha miundombinu mitambo ya maji ambayo imechakaa.

Katika kutekeleza miradi ya maendeleo pia Mhandisi Bwire amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha Sh. 35.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa tenki kubwa la maji sehemu ya Bangulo kwa ajili ya kupunguza changamoto ya maji.

About The Author

error: Content is protected !!