March 26, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Faru weusi waongezeka kwa 40% Ngorongoro

 

MAMLAKA ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) imefanikiwa kudhibiti ujangili wa wanyama pori na kusababisha kuongezeka kwa asilimia 40 ya faru weusi katika hifadhi hiyo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa na Kamishina wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Elirehema Doriye wakati wa kutoa taarifa ya maendeleo kwa miaka 4 ya utawala wa Serikali iliyopo madarakani katika ukumbi wa mikutana wa Habari Maelezo Jijini Dodoma.

Dk. Doriye amesema kuwa kutokana na kupambana na majangili kwa kiasi kikubwa kwa kipindi cha miaka 4 ya utawala wa serikali ya awamu ya sita faru weusi wameongezeka na kufikia asilimia 40 tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma.

Pia amesema kuwa kwa sasa hata simba wameongezeka na kufikia 188 kwenye hifadhi hiyo na tembo kuongezeka kutoka 800 hadi 1,300.

Akizungumzia mafanikio katika sekta utalii amesema kuwa hifadhi ya Ngorongoro ni maeneo yanayotembelewa na watalii wengi nchini kutokana na vivutio vyake kuwa ni vya kipekee.

Anasena kuwa takwimwi zinaonesha kati ya Julai 2021 hadi Februari 2025 jumla ya watalii 2,916,540 wametembelea vivutio vya utalii ndani ya hifadhi ya Ngorongoro.

Dk. Doriye amesema katika kipindi kama hicho mapato Sh. 693.9 bilioni yamekusanywa na kuingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali.

About The Author

error: Content is protected !!