
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na dLab inaendelea kuwawezesha wasichana wenye umri wa miaka 14-18 kwa ujuzi wa STEM kupitia programu ya ‘Code Lie A Girl’. Mpango huu umewawezesha zaidi ya wahitimu 3,000 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma, na Mwanza. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hafla ya mahafali iliyofanyika jijini Dar es Salaam iliongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza na wanafunzi na kuwakabidhi zawadi wahitimu huku akisisitiza dhamira ya Vodacom ya kuwawezesha wasichana kwa ujuzi wa programu (coding) na uvumbuzi.
Programu hii pia inahimiza ujumuishi kwa ushirikishaji wa wasichana wenye ulemavu, ikionyesha azma ya Vodacom ya kuziba pengo la kijinsia katika teknolojia ya kidijitali.

ZINAZOFANANA
Hadithi ya Mabingwa: Chelsea na Safari ya kutwaa Ubingwa wa Dunia
Buku moja tu, yamfanya Derick kuwa bingwa
NBC yazindua Msimu wa Pili wa Kampeni ya NBC Shambani kuhamasisha kilimo cha kahawa Ruvuma