March 26, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Bodi ya Ligi: Mchezo upo palepale, Yanga hawachezi siku nyingine

Steven Mnguto, Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) limesisitiza kuwa mchezo wa Yanga dhidi ya Simba upo palepale na hakuna sababu yoyote ya kuhairisha mechi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wakati Bodi ya Ligi ikisisitiza mchezo upo palepale, uongozi wa klabu ya Yanga umesema watapeleka timu uwanjani kwa ajili ya mechi hiyo na hawako tayari kucheza siku nyingine yoyote tofauti na leo.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mawasiliano ya Bodi ya Ligi, imeeleza kuwa wamepokea barua ya malalamiko kutoka kwa klabu ya Simba kuhusu changamoto zilizojitokeza kabla ya mchezo na tayari wanazifanyia kazi na hatua za haraka kufanyia uchunguzi tukio hilo la kuzuiwa kufanya mazoezi.

TPLB wanasema pamoja na changamoto hizo, wanapenda kuwajulisha umma kuwa kwa mujibu wa kanuni ya 15(10) ya Kanuni za Kigi Kuu Bara inasema; ‘timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu ina wajibu wa kushiriki michezo yote iliyoratibiwa na kuandaliwa na TFF bila kukosa, isipokuwa kutakuwepo na sababu maalum zilizoidhinishwa na Shirikisho.

Aidha kukosa kushiriki mchezo husika kunaweza kupelekea adhabu kulingana na Kanuni ya 16(1) inayohusu maamuzi dhidi ya timu zisizotii ratiba za ligi.

Pia, kwa mujibu wa Kanuni 17(45) inayotaja haki ya kufanya mazoezi uwanjani, tunahakikisha masuala hayo yanafuatiliwa kwa kina na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wahusika wa uvunjifu wa kanuni hizo.

Hivyo bhasi, kwa kufuatia kanuni za Shirikisho, tunawaagiza kuendelea na mchezo kama ulivyopangwa ili kuheshimu ratiba ya Ligi Kuu ya NBC na kuzingatia maslahi ya mashabiki, wadhamini na ligi kwa ujumla na malalamiko ya changamoto zilizojitokea zitafanyiwa kazi kwa wakati unaofaa.

TFF itaendelea kujitahidi kuhakikisha ligi inaendeshwa kwa haki na uwazi kwa kuzingatia kanuni zilizopo, Tunasihi mshirikiane kwa dhati ili kuhakikisha mchezo huo unachezwa kwa amani na kufanikisha ligi bora zaidi.

Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Andre Mtine

Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Andre Mtine, inasema wanapenda kuutaarifa umma kuwa mchezo wao dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika leo tarehe 8 Machi 2025, hakuna mabadiliko.

Inaeleza kuwa Yanga kama wenyeji wa mchezo huo wanaamini taratibu zote za mchezo kama inavyoelekezwa kwenye kanuni ya Ligi Kuu ya NBC zipo sawa na maandalizi yote yamekamilika.

Uongozi wa Yanga utapeleka timu uwanja wa Benjamin Mkapa kama inavyoelekezwa kwenye kanuni na hawatakuwa tayari kucheza mchezo huo siku nyingine tofauti na leo.

Taarifa hiyo imewaalika uwanjani wanachama, mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo na wadau wengine waliosafiri kutoka mikoani, nchi za jirani na sehemu mbalimbali duniani kote kuja kushuhudia mchezo huo mkubwa.

About The Author

error: Content is protected !!