
KLABU ya Soka ya Simba haitashiriki mchezo wa leo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga kufuatia kuzuiliwa kuizuiliwa kufanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salasm … (endelea).
Mchezo ulipangwa kufanyika jii leo tarehe 08 Machi 2025, kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Katika Taarifa yao waliyotoa kwa Umma, klabu hiyo imeeleza kuwa Meneja wa Uwanja huo aliarifiwa kwamba hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi kufanyika bila maelekezo ya kamishna wa mchezo, licha ya kamishna wa mchezo kufika mabaunsa wa klabu ya Yanga walivamia msafara wa Simba huku wakiendelea na vurugu.
Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa, kwa mujibu wa kanuni ya 17(45), ya kanuni ya Ligi Kuu Bara timu ngeni ina haki ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa mechi angalau mara moja kabla ya siku ya mchezo katika muda tarajiwa wachezo husika, licha ya Simba kufika Uwanjani kwa muda husika.
ZINAZOFANANA
Mwenezi Bawacha ashambuliwa mlinzi, Polisi wafunguka
Hatua za msajili analenga kuinyamazisha ajenda ya Chadema
NBC yashiriki uzinduzi uwanja mpya wa Singida Black Stars