March 26, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

TONE TONE ya Chadema yafika Mil 64

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa

 

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Amani Golugwa, amewahukuru wana-Chadema na watanzania wote kupitia kampeni ya ‘Tone Tone’ wameweza kuchanga jumla ya Sh. 64,315,150 tangu kuanzishwa kampeni hiyo, fedha itakayosaidia uendeshwaji wa shughuli za chama. Anaripoti Apaikunda Mosha. Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari tarehe 03 Machi 2025 katika Makao Makuu ya CHADEMA, Mikocheni, Dar es Salaam, Golugwa amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuendesha shughuli za chama aidha, dhamira ya Chama hicho ni njema ya kuhakikisha Taifa letu linakuwa na haki na chaguzi zenye mfumo wa kuaminika.

Amesema kuwa kila baada ya siku saba kamati ya chama itakuwa inatoa taarifa ya mapato hayo, hivyo kwa mujibu wa taarifa ya sasa, hadi kufikia tarehe 1 Machi 2025, fedha zilizokusanywa kupitia akaunti ya NMB fedha zilizokusanywa ni Sh. 16,858,461, huku michango kupitia namba ya M-PESA (0744446969) iimefika Sh. 3,997,109.

Pia, kupitia mfumo wa kulipa bili kwa M-PESA, chama kimepokea Sh. 5,785,670, wakati njia ya Mix Bill kupitia mtandao wa Mix by Yas imekusanya Sh. 1,700,000.

Golugwa amekiri kutokea kwa changamoto katika baadhi ya mifumo ya kuchangia, ambapo watumaji waliambiwa imejaa ikiwemo namba ya M-PESA, (0744446969) na tayari wamewasiliana na mamlaka husika ili kufanyiwa marekebisho, hivyo hatua za kuzitatua zinaendelea ili kumaliza tatizo hilo.

“Takwimu zinaonesha kuwa kuna kiwango kikubwa cha fedha ambacho kingeweza kuzidi Shilingi milioni 150 hadi 200, lakini mifumo ya malipo ulikuwa unawaonyesha wachangiaji umejaa, hata hivo mamlaka husika inashughulikia tatizo hilo ili wachangiaji waendelee kuchangia ili kazi iweze kufanyika.” amesema Golugwa.

Amesema kwa muitikio huu itasaidia kuongeza hari ya uwajibikaji wa viongozi hao, hivo ili kila mtu ashiriki wametengeneza njia nyingine kama fursa kwa watanzania kushiriki kuchangia, Golugwa ametangaza njia ya kuchangia kupitia programu ya Sim Banking ya CRDB kwa malipo ya kujirudia (subscription payments) kwa kila baada ya muda.

Aidha amesema kwa njia ya M-PESA unaweza kufanya malipo ya kujirudia kwa walio na akaunti zao. Na kwa watumiaji wa mitandao mingine bado mfumo huo haujawekwa. Aidha ametoa mwongozo wa utumaji wa fedha hizokupitia mitandao mingine.

Golugwa ametangaza kuanza kwa mikutano ya hadhara hivi karibuni, ili kuwaunganisha watanzainia na kuwajulisha mambo ambayo wanatamani kuyafahamu, huku kazi hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu pamoja na Makamu wake, John Heche.

“Ziara hiyo itaanza nyanda za juu katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara kabla ya kuendelea katika maeneo mengine kwa kipindi kisichopungua siku 48 na tutazunguka na kuzungumza mambo ambayo tunaamini katika kipindi na wakati huu wananchi wanahitaji kuyasikia na mathalani na kuyachukulia hatua,” amesema Golugwa.

About The Author

error: Content is protected !!