
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, ameweka wazi changamoto ambazo wafanyakazi wa umma wanapitia kutokana na mfumo mbovu wa utendaji kutoka kwa waajiri wao. Anaripoti Apaikunda Mosha, Dodoma … (endelea).
Akizungumza katika kikao kazi cha Wairi wa Utumishi na wakuu wa taasisi za umma leo Jumatatu tarehe 3 Machi 2025, Sangu amesema malalamiko kwa baadhi ya wafanyakazi ni mengi kutokana na mapungufu mengi yaliyo katika utawala na usimamizi wa rasilimali watu.
Amesema malalamiko hayo yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi kwa sababu yapo kwa dhamana yao, aidha malamiko hayo hayashughulikiwa kwa wakati hadi yanasababisha watumishi hao kulalamika jambo linaloweza kushusha morali ya kufanya kazi na kuathiri utoaji wa huduma kwa wananchi.
Ameeleza kuwa licha ya kufanyika kwa kikao jijini Dodoma mwaka 2023 kwa watumishi wa taasisi/ halmashauri kufuatia agizo la Rais juu ya kushughulikia maswala ya upandaji madaraja kwa watumishi wa umma bado kumekuwa na malalamko mengi kuwa mamlaka za ajira hazishughulikii matatizo hayo kwa wakati.
“Niimenda kwenye baadhi ya Halmashauri, mtumishi anakidhi vigezo vya kupandishwa cheo lakini jambo lake limewekwa na halishughulikiwi kwa maana ya kuletwa mahali husika, ofisi ya Rais na utumishi na nilipofuatilia nimekuta tu ni watu kutokuwajibika na kwa masikitiko makibwa lawama zote akifika mtumishi anaambiwa jambo lako limekwamia TAMISEMI au utumishi,” amesema Sangu.
Aidha, Sangu amesema Changamoto nyingine ni malimbikizo ya mshahara, amesema mamlaka za ajira hazishughulikii madai ya wafanyakazi na malimbikizo ya mishahara yao, na hata ikishughulikia hawamalizi kikamilifu kwa sababu yanapelekwa utumishi yakiwa na kasoro na yakirudishwa yanakaa mda mrefu.
Akielezea kuhusu suala la uhamisho Sangu amesema baadhi ya watumishi wameomba uhamisho kwa muda mrefu na watendaji (waajiri) hawajarudisha majibu ya kukataliwa au kukubaliwa jambo linalomfanya mtumishi kubaki dilemma anapoambiwa jambo lako liko ofisi za utumishi.
Ameeleza ambavyo mashauri mengi yamekuwa hayaendeshwi vizuri pale mtumishi anapoona hajaridhishwa najambo lake la kinidhamu na anataka kukata rufaa, anapofika Tume ya utumishi wa umma wanawaelekeza maafisa usajili waanze upya mashauri hayo, maafisa usajili wamekuwa wakigoma kuanza upya, kitendo kinachoashiria kuwa hawaheshimu sheria zilizopo bali wanafuata hisia binafsi.
“Pia wapo baadhi ya wa ajiri wanaoshindwa kuwapa mafunzo elekezi vijana wa ajira za mara ya kwanza, vijana wengi wamekua wakijiongoza na kujielekeza wenyewe kitu kinachosababisha kuwepo kwa malalamiko mengi kwasababu ya kukosa mwongozo au maelekezo ya ufanyaji kazi,” amesema Sangu.
Aidha, Sangu amesema kuwa maelekezo muhimu kwa washiriki yatatolewa kuweka maazimio ya kiutendaji, kwa lengo la kuboresha zaidi utawala na rasilimali watu katika utumishi wa umma pamoja na uzingatiaji wa sheria na miongozo ya utendaji kazi.
ZINAZOFANANA
Tundu Lissu apinga kesi yake kuahirishwa tena
Idadi ya waliofariki ajali ya Same yafikia 39
DAS Kinondoni aipongeza MONTI International kwa kuibua, kulea vipaji vya watoto