SERIKALI imewajengea uwezo wataalam 2,980 kutoka vituo 710 vya afya nchini ili waweze kutoa huduma za afya ya akili katika maeneo yao ikiwa ni hatua madhubuti ya kukabiliana na changamoto za upungufu wa wataalam wa afya ya akili nchini pamoja na kuwaajiri watumishi katika sekta hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Jesca Jonathani Msambatavangu, Bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel amesema kuwa kwa mwaka 2024, Serikali imeajiri jumla ya watumishi 56 wapya katika Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe.
Aidha, katika juhudi za kupunguza uhaba wa wataalam wa afya ya akili, Serikali imeendelea kutoa fursa za mafunzo kwa madaktari, ambapo kwa kipindi cha miaka mitano (2020-2024), jumla ya madaktari 61 wamepata nafasi ya kusomea udaktari bingwa wa afya ya akili pamoja na ubingwa bobezi katika fani hiyo.
Dk. Mollel ameongeza kumekuwa ma kuimarika kwa mfumo wa elimu ya afya ya akili, sambamba na kuongezangeza idadi ya vyuo vinavyotoa shahada ya uzamili ya afya ya akili kutoka kimoja mwaka 2019 hadi viwili ifikapo mwaka 2025.
ZINAZOFANANA
Mwabukusi: TLS siyo chama cha kulambishwa asali
Polisi wakwama, mwakilishi Wingi aachiwa huru
Askari wawili JWTZ wapoteza Maisha Goma, DR Congo