January 21, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Dk. Faustine Ndungulile afariki dunia

 

MBUNGE wa Jimbo la Kigambo (CCM) na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Faustine Ndungulile amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba 2024, nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ,,, (endelea).

Taarifa ua kifo chake imethibitishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Akson.

“Nimepokea kwa masikito makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Dunia (WHO), kanda ya Afrika Mheshimiwa Dk. Faustine Ndungulile”

“Kwa niaba ya Bunge natoa pole kwa Familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote.” Alisema Dk Tulia

Aidha katika taarifa yake imeeleza kuwa, Ofisi ya Bunge kwa Kushirikiana na Familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitatolewa.

Dk Ndungulile amefariki Dunia ikiwa zimepita siku 90 Toka alipoteuliwa kuwa mkurugenzi wa (WHO) kwa Kanda ya Afrika tarehe 27 Agosti 2024.

About The Author

error: Content is protected !!