NYUMBA ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Marndeleo (Chadema), Tundu Lissu, inadaiwa kuzimgirwa na Polisi. Anaripiti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea).
Taarifa kutoka mitandao ya kijamii ya Chadema zinaonyesha picha na video zinazodaiwa kupigwa nyumbani kwa kiongozi huyo, wakionekana maofisa wa Polisi waliovalia sare waliwa wamezingira nyumba yake.
MwanaHALISI Online limeshindwa kuwapata viongozi wa jeshi hilo kuthibitisha taarifa hizo. Linaendelea iufuatilia.
Aidha, haijaweza kufahamika mara moja iwapo Lissu yumo ndani ya makazi hayo au hayumo.
Haya yanajiri wakati chama chake, kimeitisha maandamano jijini Dar es Salaam, leo Jumatu, kupinga kushamiri kwa vitendo vya utekaji, utesaji na mauaji, yaliyorejea kwa kasi kwa siku za karibuni.
Jana mwandishi wa MwanaHALISI alielezwa na mwanasiasa huyo kuwa atachukua kila tahadhari kuhakikisha anashiriki maandamano hayo.
“Ninajua kuna mkakati wa Polisi wa kuja kunizuia kushiriki maandamano ya kesho. Nimejipanga kunasua mtego wao,” alisema Lissu, mmoja wa wanasiasa machachari nchini.
ZINAZOFANANA
Mtanzania abainika kuambukizwa Mpox
Boni Yai aruka kihunzi, asema ameshuhudia mengi gerezani
Boni Yai ashinda uchaguzi Kanda ya Pwani akiwa gerezani