KATIBU Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, amedai kuwa kuna mkakati wa kuwapo mapandikizi yalioandaliwa na serikali, kuvuruga maandamano yao. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Katika ujumbe wake wa maandishi wa mapema leo Jumatatu, Mnyika anasema, “Nimepata taarifa ya kuwapo vijana walioandaliwa kushambulia Polisi. Lengo ni kuonekana Chadema wameanzisha fujo. Tuwadhibiti mapema.”
Mnyika amesema, ni muhimu kwa wafuasi wote wa chama chake, kufika kwa wakati kwenye maeneo ambayo maandamano yamepangwa kuanzia, ikiwamo Magomeni Mapema na Ilala Boma.
“Ni maombi yangu kwenu wote, tufikir saa 3 kamili asubuhi. Tunaanzia maandamano yetu Magomeni kuelekea Ilala Boma, tutakoanzia maandamano yetu kuelekea Mnazi Mmoja,” amesisitiza.
ZINAZOFANANA
Mtanzania abainika kuambukizwa Mpox
Boni Yai aruka kihunzi, asema ameshuhudia mengi gerezani
Boni Yai ashinda uchaguzi Kanda ya Pwani akiwa gerezani