December 26, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mbowe: Tutawaburuza mahakamani Sisti Nyahoza, Awadhi Haji

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, CP - Awadh Haji

 

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema wanatarajia kuwaburuza mahakamani Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo, CP – Awadh Haji pamoja na Msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisti Nyahoza ili kuwawajibisha kutokana na madhila waliyotendewa viongozi na wafuasi wa chama hicho. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Pia amesema Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, Tundu Lissu ndiye atakayeongoza jopo la mawakili katika kesi hiyo hasa ikizingatiwa sasa amerejeshewa leseni yake ya uwakili na kwa siku nyingi hajaonekana mahakamani.

Mbowe ametoa msimamo huo leo Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano jijini Dar es Salaam kuhusu tukio la viongozi wakuu na wafuasi zaidi ya 520 waliokamatwa mapema wiki hii kwa tuhuma za kukaidi agizo la kutofanya kongamano la maadhimisho ya siku ya vijana duniani.

Kongamano hilo lilipaswa kufanyika tarehe 12 Agosti mwaka huu mkoani Mbeya, lakini badala yake viongozi wakuu wa chama hicho walikamatwa na kudaiwa kupigwa akiwamo Mwenyekiti wa Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi anayedaiwa kuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akifafanua zaidi kuhusu kesi hiyo, Lissu amesema watashtaki Sisti na Awadhi watawashtaki kwa kuvunja mkutano huo wa Bavicha bila sababu, viongozi na wanachama kupigwa, kukamatwa, kufungwa, udhalilishaji na uharibifu wa mali za chama.

About The Author

error: Content is protected !!