MADIWANI wa Halmashari ya Manispaa ya Morogoro wameitaka Halmashauri hiyo kuhakikisha inanunua Greda la kuchonga barabara kabla ya Agosti 30 mwaka huu ili kutowakwamisha kwenye uchaguzi hapo mwakani. Anaripoti Christina Cosmas, Morogoro … (endelea).
Madiwani hao akiwemo Samuel Msuya wa kata ya Mbuyuni wamesema hayo kwenye kikao robo ya mwisho ya baraza madiwani kinachofanyika kwenye ukumbi wa manispaa hiyo.
Msuya anasema changamoto ya barabara iliyopo kwa sasa kwenye karibu kata zote za Manispaa ni kubwa sababu barabara karibu zote hazipitiki na wanashindwa ya kuwaleza wananchi wao ambapo waliazimia kununua Greda ili kusaidiana na wakala wa barabara nchini (TARURA) kutatua changamoto hiyo.
Anasema waliazimia ifikapo Agosti 30 greda hilo liwe tayari kwa uzinduzi baada ya kukamilika manunuzi yake.
Naye Diwani wa kata ya Lukobe Selestin Mbilinyi alisema katika kikao cha awali walikubaliambiwa zimebaki shilingi Milioni 550 kati ya milioni 700 walizochanga ambapo waliomba kuongezwe fedha za bakaa ili kuweza kununua Greda hilo.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Mhandisi Pascal Kihanga alisema upembuzi kamili wa ununuzi wa greda kutoka kwa mhandisi wa Manispaa ulibaini kuwa manunuzi ya greda lenye thamani ya shilingi Milioni 700 hayatakidhi mahitaji kutokana na greda hilo kuwa katika mfumo usiokubalika.
Meya huyo alisema Greda hilo litanunuliwa kwa muda muafaka uliokubaliwa kwa kiasi cha shilingi Bilioni 1.2 badala ya shilingi Milioni 700 iliyotengwa.
ZINAZOFANANA
Mpina amvaa Bashe kivingine
CHADEMA: Maandamano yako palepale
Prof. Tibaijuka: Wizi wa kura upo