Mafuvu ya watu 17 yaliyokuwa yamezikwa ndani ya makasha ya chuma yamefukuliwa katika jengo linalodaiwa kuwa la kuabudia katikati mwa Uganda. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa… (endelea).
Mafuvu hayo yamebainika baada ya watoto waliokuwa wakitafuta kuni nje ya kijiji cha Kabanga jirani na mji wa Mpigi, takribani kilometa 40 magharibi mwa mji mkuu Kampala, kugundua makasha hayo juzi Jumatatu.
Msemaji wa polisi wa eneo hilo, Majid Karim amesema wakazi wa eneo hilo waliwaambia maafisa wa polisi kuwa kulikuwa na maboksi yaliyokuwa na vitu vinavyoonekana kuwa mafuvu yaliyozikwa ndani ya jengo la ibada.
“Haraka tuliingia na kuchimba eneo hilo, na mpaka sasa tumepata mafuvu ya binadamu 17.
“Tunafanya uchimbaji zaidi kuhakikisha hakuna mafuvu zaidi kuliko haya tuliyoyagundua” alisema.
Aliongeza kuwa mabaki hayo yanafanyiwa uchunguzi kujua umri wao na jinsia, pamoja na kujua lini yalifukiwa.
Amewasihi watu kuwa watulivu, akisema baadhi ya wakazi wameondoka kwa woga.
Jengo hilo linadaiwa kuwa mali ya Tabula Bbosa Lujja, mshukiwa wa mauaji ya kiongozi wa kimilika katika kabila la Buganda, Daniel Bbosa aliyeuawa tarehe 25 Februari mwaka huu.
Kabla ya mmiliki wa jengo hilo atoweke kutokana na tuhuma hizo za mauaji, majirani wameeleza kuwa lilikuwa likitumiwa na watu kwa kufanyia ibada.
ZINAZOFANANA
Korea Kusini lawamani kukandamiza uhuru wa dini
Chama tawala Botswana chaangushwa vibaya
Mtaalamu wa kemia kiongozi mpya Hezbollah