QATAR leo inatarajiwa kufanya mazishi ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, baada ya mauaji yake yaliyotokea huko Tehran Iran, katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na Israel Haniyeh atazikwa katika maziara ya Lusail, kaskazini mwa Doha baada ya sala itakayofanywa katika msikiti mkubwa nchini Qatar wa Imam Muhammad bin Abdul Wahhab. Hamas imesema kwamba viongozi wa Kiarabu na Kiislamu, pamoja na wawakilishi wa makundi mengine ya Palestina na raia, watahudhuria mazishi hayo. Kuuwawa kwa Haniyeh kulifanyika saa chache baada ya Israel kufanya shambulizi kusini mwa Beirut na kumuua Fuad Shukr, kamanda wa kijeshi wa kundi la Hezbollah lililo na mafungamano na Hamas. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Watoto waliokuwa wanaokota kuni wabaini mafuvu 17 kanisani M23 wateka mji wa mpakani na Uganda