October 31, 2024

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kiongozi mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh ameuawa

TAARIFA iliyotolewa na Hamas imesema kuwa Haniyeh ameuawa katika shambulio lililofanywa na Wazayuni (Israel) mjini Tehran, Iran. Inaripiti Mitandao ya Kimaraifa.

Katika taarifa yake Jumatano asubuhi, Hamas ilisema Haniyeh aliuawa katika uvamizi wa Israel alipokuwa ziarani Tehran kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Masoud Pezeshkian.
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Iran pia limethibitisha kifo chake

Wanajeshi wa Israel na viongozi wakuu ndani ya serikali yake bado hawajajibu madai hayo.

About The Author