CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa taarifa kuwa kesi ya madai inayowahusu Saidi Issa Mohammed pamoja na wenzake wawili dhidi ya Registered Trustees wa chama hicho na Katibu Mkuu wake, imepangwa kutajwa rasmi kesho 22 Aprili 2026.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shauri hilo litasikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, kuanzia saa 03:15 asubuhi mbele ya Jaji D. Ngunyale.

Imeelezwa kuwa utaratibu wa usikilizwaji wa kesi hiyo utafanyika kwa njia ya video conference, ikiwa ni sehemu ya matumizi ya teknolojia katika shughuli za mahakama.

Chadema imesisitiza kuwa inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo, na itaendelea kutoa taarifa zaidi kadri hatua za kisheria zitakavyoendelea.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!