APPLE Music imemtangaza muimbaji na mtunzi wa nyimbo za injili kutoka Tanzania, Moses Luka, kuwa msanii wa awamu mpya kujiunga na mpango wake wa kukuza vipaji wa ‘Up Next’ katika ukanda wa Afrika Mashariki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). Akizungumzia mpango huo, Moses Luka amesema, ana furaha isiyo na kifani kutokana na kupata bahati katika jukwaa hilo kubwa la muziki duniani. “Ninahisi kuheshimiwa sana kuchaguliwa katika kampeni ya Apple Music Up Next Afrika Mashariki. Wasaa huu haumaanishi tu ushindi wa safari yangu binafsi, bali pia ni ishara ya sauti na roho ya kizazi kipya cha wasanii wa Afrika Mashariki kilicho tayari kusimulia hadithi zao kwa dunia nzima,” Moses Luka ameimbia Apple Music. Akaongeza: “Mwaka 2026, mashabiki zangu watarajie muziki wenye uzito zaidi, hisia za ndani, wenye dhamira na unaogusa dunia huku ukiwa umesimama katika imani, utamaduni na uhalisia. Nimejipanga kusukuma mipaka ya ubunifu na kujenga mahusiano yenye maana pamoja na timu yangu.” Akizaliwa na kukulia Tanzania, Moses Luka alipata umaarufu kitaifa baada ya kushinda shindano ya Bongo Star Search 2025, moja ya mashindano makubwa ya kusaka vipaji vya muziki nchini. Baada ya mafanikio hayo, alifanya uamuzi wa makusudi kuhamia kwenye muziki wa Injili, akasaini na OSPO Music Group na kuelekeza sanaa yake katika huduma kupitia nyimbo zenye msingi wa imani, kusudi na ukweli wa kiroho. EP yake ya kwanza, Moses Lu, inaashiria hatua muhimu katika safari yake ya muziki, ikichanganya Injili ya kisasa na ladha ya muziki wa Kiafrika ili kutengeneza uzoefu wa kusikiliza wenye hisia na unaotia moyo. Ikiwa imepikwa kugusa mada za kutia matumaini, shukrani, uvumilivu na kumtumainia Mungu, kazi hiyo inaakisi safari yake ya kiimani huku ikionesha ukuaji wake kama mwimbaji na msimuliaji wa hadithi. Kama msanii mpya wa Up Next Afrika Mashariki, Moses Luka atajumuishwa kwenye orodha ya nyimbo ya Up Next ya Apple Music: https://apple.co/3eITdJd. Orodha hiyo huangazia vipaji vinavyochipukia vilivyochaguliwa na wahariri wa Apple Music kutoka kote duniani, wakiwawakilisha wasanii wanaosukuma mipaka ya ubunifu na wenye uwezo wa kufikia hadhira ya kimataifa. Orodha kubwa ya wasanii waliowahi kushiriki Up Next duniani inajumuisha vipaji vilivyotajwa kuwania tuzo za Grammy na vinavyokubalika kimataifa kama 6lack, Daniel Caesar, H.E.R., Greta Van Fleet, Khalid, Amy Shark, Billie Eilish, Sabrina Claudio, Sigrid, Mr Eazi, Stefflon Don, Bad Bunny, Juice WRLD, Bazzi, Jax Jones, NCT 127, Summer Walker na Tierra Whack. Wengine ni Dean Lewis, Pink Sweat$, Koffee, Megan Thee Stallion, Burna Boy, Clairo, Lunay, Jessie Reyez, Orville Peck, Victoria Monét, Ingrid Andress, Conan Gray, Don Toliver, Rema, BENEE, Holly Humberstone, Natanael Cano, Givēon, beabadoobee, Arlo Parks, Tate McRae, Foushee na Tems. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Chelsea kulipa kisasi ugenini dhidi ya Brighton?