MAHAKAMA ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano, imekiondolea zuio la kufanya shughuli za kisiasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea). Katika uamuzi wake uliosomwa leo Jumatano, tarehe 15 Aprili 2026, Mahakama imesema zuio hilo, limewekwa kinyume na sheria na hivyo, linapaswa kuondoka. “Maamuzi yametoka na Mahakama ya Rufaa imeamua kuondoa zuio dhidi ya chama ya kufanya shughuli zake za kisiasa,” ameeleza Dickson Matata, wakili wa Mahakama Kuu na Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho. Uamuzi huo wa Mahakama ya Rufani, umetokana na hatua ya Chadema kumuomba Jaji Mkuu, kutumia madaraka yake, kupitia Mahakama ya Rufani, kuangalia mwenendo wa kesi iliyoendeshwa na Jaji Hamidu Mwanga, aliyekuwa akisikiliza kesi ya mgawanyo wa mali, iliyofunguliwa na Said Issa Mohammed na wenzake wawili. Aidha, majaji wa Mahakama ya Rufani wameagiza faili la kesi hiyo, lipelekwe kwa jaji mwingine ambaye ataanza kwa kuangalia uhalali wa shauri lenyewe. Kwa uamuzi huo, Chadema sasa iko huru kuendelea na shughuli zake za kisiasa. Amri ya kukizuia kufanya shughuli hizo, ilitolewa Aprili mwaka jana. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Erasto Masalu See author's posts Post navigation Nchimbi awataka Mabalozi wateule kuimarisha Uhusiano ya Kimataifa