UONGOZI wa Simba SC umemrejesha mshambuliaji wake raia wa Ghana, Jonathan Sowah, lakini kwa sharti kwamba afanye mazoezi na timu ya vijana ya klabu hiyo chini ya umri wa miaka 20 (Simba U20).Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam …(endelea). Sowah alisimamishwa mapema mwaka huu wakati timu ilipokuwa Dodoma ikijiandaa na mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi Februari kabla ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji FC. Katika kipindi hicho, alirudishwa Dar es Salaam na tangu wakati huo hajacheza mechi yoyote ya ligi au mashindano. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa mchezaji huyo alifika mbele ya kamati ya nidhamu ya klabu na kupatikana na hatia kwa baadhi ya makosa yaliyokuwa yakimkabili. Ally alieleza kuwa kamati hiyo imeamua Sowah afanye mazoezi na timu ya vijana chini ya uangalizi wa karibu. Kurudi kwake kwenye kikosi cha wakubwa kutategemea mwenendo wake na kama kamati itaridhika na maendeleo yake. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Rais Mwinyi akagua mradi wa mji wa AFCON Fumba CRDB yatangaza washindi wa safari ya Fainali ya Kombe la Dunia Marekani