CHINA imekosoa vikali hatua ya Marekani ya kuanzisha udhibiti wa meli zinazoingia na kutoka katika bandari za Iran, ikiitaja kuwa ni hatua hatari na isiyowajibika ambayo inaweza kuongeza mvutano wa kisiasa na kudhoofisha makubaliano dhaifu ya usitishaji wa vita.Anaripoti mwandishi wetu, Dar es Salaam …(endelea). Wizara ya Mambo ya Nje ya China kupitia msemaji wake Guo Jiakun imesema hatua hiyo iliyoanza Jumatatu imekuja siku moja baada ya mazungumzo ya amani kati ya Marekani na Iran kuvunjika nchini Pakistan. Amesema badala ya kutuliza hali, udhibiti huo unaweza kuchochea mzozo mpya katika eneo la Mashariki ya Kati. Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na taarifa zinazoeleza kuwa China inadaiwa kuandaa mifumo mipya ya ulinzi wa anga kwa Iran, madai ambayo Beijing imeyakanusha na kuyaita ya kutungwa. Ripoti hizo zilimfanya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kutoza ushuru wa asilimia 50 bidhaa za China endapo itatoa msaada wa kijeshi kwa Tehran. Guo amesema iwapo Marekani itaendelea kutumia madai hayo kama kisingizio cha kuongeza ushuru dhidi ya China, basi Beijing itachukua hatua kali za kujibu. Kauli hiyo inaashiria kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara kati ya mataifa hayo mawili makubwa duniani. China ni mnunuzi mkubwa wa mafuta ya Iran, hivyo ina maslahi ya kuona mzozo huo ukimalizika haraka na soko la dunia kurejea katika utulivu. Wachambuzi wanasema hatua yoyote inayozuia usafirishaji wa mafuta kutoka Iran inaweza kusababisha bei za nishati kupanda zaidi na zaidi duniani. Takwimu zinaonesha kuwa mwezi Machi Iran ilisafirisha mapipa milioni 57.9 ya mafuta, ikiwa ni moja ya miezi yake mikubwa zaidi ya mauzo licha ya changamoto za usalama katika Mlango wa Hormuz. Hali hiyo inaonesha umuhimu wa Iran katika soko la kimataifa la mafuta. Share this… Facebook Pinterest Twitter Linkedin Whatsapp About The Author Fedrick Gama See author's posts Post navigation Iran yaonya: “bado hatujaonesha nguvu zetu halisi za kijeshi”