March 27, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Lukuvi atakumbukwa kama nguzo muhimu wa familia

Thom Lukuvi

 

WILLIAM Lukuvi, aliyekuwa mbunge wa jimbo la Isimani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), atakumbukwa kama nguzo muhimu aliyekuwa akishikilia mshikamano wa familia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mwanasiasa huyo anayetarajiwa kupumnzishwa kijijini kwao Idodi Iringa vijijini 31 Machi, alifariki dunia Jumatano iliyopita, mkoani Dodoma.

Akizungumza nyumbani kwao mtoto wa kaka yake na marehemu Lukuvi Thom Lukuvi anaeleza kuwa marehemu hakuwa tu kiongozi wa kisiasa, bali pia mlezi na mshauri aliyekuwa tayari kusimama na mtu yeyote aliyehitaji msaada.

Amesema katika maisha yake ya kila siku, William Lukuvi alijulikana kwa moyo wake wa kusaidia wengine somo ambalo amewaachia kwa wanafamilia

Thom amesema kuwa Familia inaeleza kuwa misingi ya haki na ukweli ndiyo iliyomuongoza katika maamuzi yake yote kwani alisimamia usawa, na haki, bila upendeleo sifa ambazo zilimtofautisha na kumfanya kuwa mfano wa kuigwa, si tu kwa familia yake bali pia kwa jamii nzima.

About The Author

error: Content is protected !!