February 20, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kardinali Pengo kuzikwa Pugu Feb 28

 

MWILI wa aliyekuwa Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo unatarajiwa kuzikwa jumamosi ya tarehe 28 Februari 2026, kwenye kituo cha hija Pugu. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Jimbo Kuu la Dar es Salaam, shughuli za kutoa heshima za mwisho zitaanza Ijumaa ya tarehe 27 Februari 2026 sambamba na ibada kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph na mwili huo kukesha kanisani hapo, na asubuhi ya tarehe 28 Feb 2026 utaelekea kituo cha hija Pugu kwa ajili ya ibada na mazishi.

Kardinali Pengo alifarika usiku wa tarehe 19 Februari 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).

About The Author

error: Content is protected !!