WASWAHILI hunena kama ulivyoawatendea mwenzako nawe utatendewa, usemi huu utathibiti kesho ambapo wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), watakapokwenda kupiga kura ya kuchagua viongozi wapya. Anaandika Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kutangaza kutoutambua uongozi wa CUF, na kutaka uchaguzi huo urejewe.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF–Bara, Magdalena Sakaya, amesema hawakubaliani na uamuzi huo na tayari wameamua kwenda mahakamani.
Sakaya amesema chama kina vyombo vyake vya maamuzi, na iwapo Msajili anaona uchaguzi wa mwenyekiti ulikuwa na dosari kwa kuwa kura hazikuzidi asilimia 50, basi hoja hiyo haina msingi. Amesema kati ya wagombea tisa, zaidi ya nusu ya kura zilipatikana kwa mujibu wa utaratibu wa chama.
Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akirejea mgogoro uliowahi kutokea kati ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba, na aliyekuwa Katibu Mkuu, Maalim Seif, ambapo Ofisi ya Msajili ilitoa uamuzi wa kumtambua Profesa Lipumba na kumkana Maalim Seif, na chama kiliridhia. Kisha akahoji kwa nini sasa CUF wanapinga uamuzi huu.
Leo tarehe 20 wajumbe wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), wameanza kujisajili majina yao ikiwa ni hatua ya mwisho ya maandalizi kabla ya kuingia ukumbini kwa ajili ya kupitisha ajenda mbalimbali pamoja na kuthibitisha majina ya makada waliokidhi vigezo vya kugombea nafasi za juu za uongozi ndani ya chama hicho.
Usajili huo ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho, tarehe 21 Februari 2026, ambapo wajumbe wanatarajiwa kushiriki mchakato wa kupiga kura utakaolenga kupata viongozi wapya wa chama.
Wakati huo huo, hali ya ulinzi imeimarishwa katika makao makuu ya chama yaliyopo Buguruni, jijini Dar es Salaam, huku askari wa jeshi la Polisi wakifanya doria za mara kwa mara kuzunguka eneo hilo ili kuhakikisha usalama na utulivu vinadumishwa wakati wote wa maandalizi ya mkutano huo.
Hatua hiyo inakuja kufuatia uamuzi wa msajili wa vyama vya siasa kutengua uchaguzi wa chama uliofanyika mwaka 2024, na kumrejesha madarakani Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa chama, sambamba na viongozi wengine watano wa juu.
Hata hivyo, maendeleo hayo yanafanyika katika mazingira ya mvutano wa ndani ya chama, ambapo CUF imeendelea kugawanyika katika makundi mawili yanayokinzana, kundi moja likitangaza nia ya kwenda mahakamani kupinga uamuzi wa msajili wa vyama vya siasa, huku kundi jingine likiendelea na maandalizi ya mkutano huo kwa lengo la kuchagua uongozi mpya.
ZINAZOFANANA
Lissu alivyombana shahidi wa 14 wa serikali, neno kwa neno
Tundu Lissu aanza kumbana shahidi wa 14
Mahkama Z’bar yatupa kesi za uchaguzi