February 6, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Mahakama Kuu Z’bar yaipiga stop ZEC kuteketeza nyaraka za uchaguzi

 

MAHAKAMA Kuu ya Zanzibar, Masjala ya Tunguu imeamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), kusitisha mpango wake wa kuharibu nyaraka za uchuguzi mkuu wa mwaka jana. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Amri hiyo imetolewa leo na Jaji  Salma Hassan,ambayo ni zuio la muda lilitokana na maombi madogo Na.18/2026.

Waombaji ni wagombea 17 wa Chama cha ACT-Wazalendo, waliopinga uchaguzi kwenye majimbo 17 ya Unguja.

Kupitia Taarifa ya Katibu wa uenezi wa chama hicho Salim Biman aliyoitoa leo amesema kuwa nyaraka zilizozuiwa kuharibiwa nia pamoja na Fomu PS, Na. 9 , fomu ya hesabu za kura Na.13B , FOMU na. 16  fomu Na. 17 B. 19 B, fomu Na. 23 pamoja na orodha ya wapiga kura ya mapema wa Jimbo la Pangawe, Malindi, KiembeSamaki, Chumbuni, Chaani, Makunduchi, Mwera, Nungwi, Tumbatu, Mkwajuni, Bumbwini, Mpendae, Mtoni, Welezo, Amani, Mwanakwerekwe, andKijini walioruhisiwa kupiga Kura siku ya mapema ya upigaji Kura (28 Oktoba, 2025)

About The Author

error: Content is protected !!