January 15, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Kesi ya uhaini ya Lissu kusikilizwa siku 26 mfululizo

Tundu Lissu akiwa mahakamani

 

ZIKIWA siku 51 tangu kuahirishwa shauri Na. 19605/2025 la uhaini linalomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mahakama Kuu, masjala ndogo ya Dar es Salaam imepanga kuikiliza shauri hilo kwa siku 26 mfululizo kuanzia tarehe 9 Februari mpaka tarehe 6 Machi 2026. Anaripoti Fedrick Gama, Dar es Salaam … (endelea).

Shauri hilo linasikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Nduguru, Jaji James Karayemana na Jaji Ferdinand Kiwonde litaendelea kwa upande wa Jamhuri kuwasilisha hoja zao dhidi ya pingamizi la Lissu.

Lissu aliibua pingamizi la uhalali wa kutumika kwa sheria ya kulinda mashahidi akidai kuwa sheria hiyo haijachapishwa kwenye gazeti la Serikali na kwamba sheria yoyote ambayo haijachapishwa kwenye gazeti hilo haiwezi kutumika.

Lissu ameibua pingamizi hilo tarehe 12 Novemba mwaka jana ambapo shahidi wa nne wa serikali ambaye ni wa siri aliyepewa jina la ‘p1’ alipotaka kuanza kutoa ushahidi wake.

Lissu alidai mahakamani hapo kuwa hata kama sheria ya ulinzi wa mashahidi ingekuwa halali kutumika basi shahidi huyo alitakiwa kuonwa na majaji lakini hata majaji wanaendesha shauri bila kumuona shahidi jambo ambalo Lissu amedai halikubaliki kisheria.

About The Author

error: Content is protected !!