Askofu Jude Ruwa'ichi
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi amewahimiza waumini wa Kanisa Katoliki kuwa waumini wa kweli na sio uumini wa kubabaisha na kudanganya. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Askofu Ruwa’ichi ameyasema hayo hii leo tarehe 10 January 2025, kwenye ibada ya kufunga Jubilei Kuu ya Mwaka 2025 (Mahujaji wa matumaini) iliyofanyika kwenye kituo cha hija Pugu.
Akizungumza na waumini kuelekea mwishoni mwa ibada Ruwa’ichi aliwaambia waumini hao kuwa wanapaswa kubaki kuwa wakotoliki wa kweli wasiwe wa kubabaisha na kupotosha.
“Ukiwa Mkatoliki simama uwe Mkatoliki kweli, usikubali kuwa Mkatoliki wa kubabaisha, Mkatoliki wa maigizo, msiwe wakatoliki wa vijora hata kama mnahongwa ela bakini kuwa wakotoliki wa kweli,” Alisema Askofu Ruwa’ichi
Askofu Ruwa’ichi ameyasema hayo kufuatia hivi karibuni kuibuka kwa kikundi cha waumini wanaojiita wakatoliki ambao kupitia video mbalimbali mtandaoni walionekana kufika kwenye Ubalozi wa Papa nchini kupeleka barua ya malalamiko kuhusu mwenendo wa Askofu Ruwa’ichi na Padri Dk. Charles Kitima katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.
Malalamiko hayo juu ya viongozi hao wa kiroho yamekuja kufuatia hivi karibuni kutaka Serikali kusimamia haki ili kuleta ustawi kwa jamii ya watanzania mara baada ya kutokea kwa machafuko ya tarehe 29 Oktoba 2025.
ZINAZOFANANA
Wanafunzi 77 wafutiwa matokeo ya kidato cha nne, ufaulu wapanda
Uwekezaji wa Samia, wanafunzi 16 wasomea Data Science na AI Afrika Kusini
Meridianbet yawakumbuka wanaopitia maisha magumu Kinondoni