KAMPUNI ya reli ya taifa (TRC), imesitisha safari zake za treleni ya kisasa, maarufu kama SGR, kati ya Dodoma na Morogoro, kuanzia leo, tarehe 31 Desemba 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa ya kampuni hiyo, iliyotolewa na mkurugenzi wake, Machibya Shiwa, imeeleza kuwa kusitishwa kwa safari hizo, kumetokana na uharibu wa miundombinu yake, kulikosababishwa na mvua.
“Kutokana na kuharibika kwa miundombinu hiyo, katika eneo la Kidete, Kilosa, mkoani Morogoro na Gedegode, Mpwapwa mkoani Dodoma, shirika linatangaza kusitisha safari zake, hadi hapo matengenezo ya eneo lililoharibika litakapofanyiwa marekebisho,” imeeleza taarifa ya mkurugenzi mkuu.
Aidha, mkurugenzi huyo amesema, kufuatia athari hizo za mvua, safari za SGR sasa zitakuwa ni kati ya Morogoro na Dar es Salaam na Dar es Salaam – Morogoro.
Amewaomba abiria wote waliopanga kusafiri kwa kutumia SGR, kubadilisha ratiba za safari zao, kutokana na mabadiliko yaliyotajwa.
Treleni ya SGR imekuwa tegemeo kubwa kwa wananchi wanaosafiri kati ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma, pamoja na mikoa mingine nchini, hasa ya Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza, Kagera na Manyara.
Kwa takribani siku tatu sasa, mikoa ya Kanda ya Kati na Nyanda za juu Kusini, zimekumbwa na mvua kubwa zilizosababisha kukatika kwa madaraja, jambo lililosababisha usafiri wa umma na binafsi, kuvurugika.
ZINAZOFANANA
Mwaka mpya umeanza kwa kishindo
Meridianbet yaleta mwanga wa mwisho wa Mwaka kwa akina kama Palestina hospitali
Matukio 5 yakukumbukwa na kutikisa zaidi 2025