SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limeomba radhi abiria wote wanaotumia huduma za usafiri wa reli zake za MGR na SGR kufuatia usumbufu walioupata abiria waliotumia usafiri wa reli siku ya tarehe 28 Desemba mwaka huu. Anaripoti Joyce Ndeki, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa tarehe 29 Desemba, 2025, TRC limeeleza kuwa ratiba za treni za SGR zitaendelea kama zilivyopangwa kwa siku ya Jumatatu,ya tarehe 29 Desemba 2025. Aidha, shirika hilo limeamua kuongeza safari za ziada ili kukabiliana na changamoto iliyojitokeza na kuhakikisha huduma kwa abiria zinaendelea kwa ufanisi.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano kwa umma wa TRC, Fredy Mwanjala, imeeleza kuwa safari za treni kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam zitafanyika saa 11:15 alfajiri, saa 12:00 asubuhi (EMU), saa 08:15 mchana, saa 09:00 mchana (EMU), saa 11:15 jioni, saa 12:00 jioni (EMU) na saa 12:40 jioni.
Kwa upande mwingine, safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma zitakuwa saa 12:00 asubuhi, saa 01:00 asubuhi, saa 02:00 asubuhi (EMU), saa 03:30 asubuhi, saa 04:30 asubuhi (EMU) na saa 12:55 jioni.
TRC imeeleza kuwa safari ya treni kutoka Morogoro kwenda Dar es Salaam itakuwa saa 03:50 asubuhi, huku safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro ikipangwa kufanyika saa 10:00 jioni.
ZINAZOFANANA
TMA yatangaza mvua kubwa zitakuja, mikoa 14 kuathirika
Mwigulu akagua uzalishaji na usambazaji maji Ruvu chini
Dk. Mohamed aendeleza mageuzi katika jamii ya Mtambwe