Harbinder Singh Sethi
MRADI wa kukwapua mabilioni ya shilingi za walipa kodi, kwa kisingizio cha kumlipa Harbinder Singh Sethi (Singasinga), sasa unakaribia kuiva, imefahamika. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Anayejiita mmiliki wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Independent Power Tanzania (IPTL), anataka kulipwa mabilioni hayo ya shilingi kwa kinachoitwa, “kupunjwa madai yake” dhidi ya shirika la umeme la taifa (Tanesco).
Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, mchakato wa serikali kumlipa Sethi, ulikuwa mbioni kukamilika; mabilioni hayo ya shilingi yanatarajiwa kuingizwa kwenye akaunti za kampuni hiyo, muda wowote kutoka sasa.
“Mchakato wa malipo upo katika hatua za mwisho. Kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa, muda si mrefu fedha hizo zitalipwa,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi serikalini.
Kiongozi kutoka wizara ya fedha anasema, “tayari kumefanyika vikao kadhaa vya majadiliano, vikihusisha watu kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali (G), Benki Kuu (BoT), Hazina, wizara ya nishati, Tanesco na IPTL, ili kuangalia jinsi ya kulipa fedha hizo bila keleke kutoka nje na uhalali wa madai hayo.”
Anasema, baada ya majadiliano marefu, wamiliki wa IPTL na serikali, wamefikia maamuzi ya kulipa takribani Sh. 380 bilioni.
Alipoulizwa ni hakikisho gani walilopata na vigezo vipi walivyotumia kuhalalisha uwapo wa deni hilo, kiongozi huyo aligoma kulizungumzia suala hilo kwa undani.
Aidha, IPTL imewasilisha serikalini madai mengine ya fidia, zinazotokana na gharama za uzalishaji wa umeme na ada za kisheria.
Kwa upande mwingine, hadi Juni 2024, IPTL ilikuwa haijarudisha serikalini dola za Marekani 148 milioni (Sh. 389.83 bilioni), zilizotokana na makubaliano ya fedha za Tegeta Escrow.
Vyanzo vya taarifa kutoka ndani ya serikali vinasema, Sethi anatumia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inayoeleza kuwa serikali inadaiwa na IPTL, takribani Sh. 238 bilioni, kutokana na mkataba wake na Tanesco.
Kati ya fedha hizo, CAG anasema, Sh. 111 bilioni, zinatokana na deni la msingi na Sh. 127 bilioni, ikiwa imepatikana kwa njia ya riba.
Serikali ilijifunga kwenye mkataba wa miaka 20 wa mauziano ya umeme wa dharura kutoka IPTL – Power Purchase Agreement-PPA), yenye makao yake makuu, Tegeta, Salasala, jijini Dar es Salaam.
ZINAZOFANANA
Kesi ya uhaini ya Lissu kusikilizwa siku 26 mfululizo
Mvutano wa kisheria wagubika Mahkama ya Z’bar
Singida waipa kongole RITA kutoa vyeti vya kuzaliwa ndani ya saa 48