MAKAMU wa Rais wa Tanzania, Balozi Emmanuel Nchimbi amesema, taifa limepata pengo kuondokewa na aliyekuwa Mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma, Jenista Mhagama. Amesema, Jenesta alikuwa kiongozi aliyeheshimika na kutumikia nchi katika majukumu mbalimbali ya kitaifa. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akitoa salamu za rambirambi alipowasili kuhani msiba nyumbani kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, leo Alhamisi, tarehe 11 Desemba , huko Itega mkoani Dodoma.
Amesema marehemu Mhagama licha ya kuwa ni alikuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, lakini pia alitoa mchango wake katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusimamia maendeleo ya mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
Makamu wa Rais ametoa pole kwa familia na waombolezaji na kuwaombea watoto wa marehemu na ndugu wa karibu, Mungu awape ujasiri wa kukubali jambo hilo na kutambua ni njia ya watu wote.
Kwa mujibu wa taarifa ya Bunge la Tanzania, Jenesta Joakim Mhagama, amefariki dunia leo mjini Dodoma.
ZINAZOFANANA
AG-SMT ageuzia kibao wapinga ubunge, ahoji Mahkama ya Z’bar
Waziri Homera azindua huduma bure za msaada wa kisheria Morogoro
Bagonza achambua wanaopinga Kanisa Katoliki