January 23, 2026

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Jenesta Mhagama kuzikwa desemba 16, Mbinga

Jenesta Mhagama

 

MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho (CCM), Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa Jumanne ya 16 Desemba 2025 katika Kijiji cha Ruanda, Mbinga mkoani Ruvuma. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).

Jenista ambaye amekuwa mbunge wa Peramiho kuanzia mwaka 2005, amefariki dunia jana Alhamisi, 111 Desemba 2025 jijini Dodoma.

Ratiba ya mazishi yake iliyotolewa usiku wa Alhamisi na uongozi wa Bunge, inaonesha Ijumaa, mwili wake utapelekwa nyumbani kwake Itega, jijini Dodoma.

Jumamosi ya 13 Desemba 2025, mwili wa Jenista utapelekwa Kanisa Katoliki Kiwanja cha Ndege itakapofanyika ibada.

Viongozi mbalimbali watahudhuria kanisani hapo wakiwemo Spika wa Bunge, Mussa Zungu, Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba na Makamu wa Rais, Emmanuel Nchimbi.

Baada ya shughuli ya hapo kanisani, mwili wa Jenista utasafirishwa kwenda Songea, Mkoa wa Ruvuma.

About The Author

error: Content is protected !!