October 25, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

UDASA yageuka mbogo, yauvaa uongozi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

 

JUMUIYA ya wasomi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA), imeonya kuwa haitawavulia wanachama wake, wataokakwenda kinyume na jumuia hiyo. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

UDASA inasisitiza kuwa imetekelezaji wabibu wake wa msingi wa kupigania uwajibikaji katika jamii ya kitaaluma, na kwamba tamko lao la tarehe 23 Oktoba, halina uhusiano na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mwenyekiti wa UDASA, Elgidius Ichumbaki, ameeleza kuwa tamko walilotoa linahimiza haki na kueleza kuwa hakuwezi kupatikana amani nchini, bila kuwapo haki.

Viongozi wetu watende haki, kwani amani haiwezi kuwepo bila watu kupa haki,” ameeleza.

Tamko hilo lilisisitiza kuundwa kwa tume ya kijaji kuchunguza matukio yote ya utekaji na kuwataka viongozi kujiepusha na kauli tata.

“Ni lazima viongozi wa umma, wajiepushe na kauli tata na matendo ya kudharau Katiba. Navyo vyombo ya ulinzi na usalama vijiepushe kutumika kisiasa,” imeeleza taarifa ya wanajumuiya hiyo.

Tamko hilo limepinga vikali na tamko lililotolewa mapema asubuhi ya leo na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kupinga kauli ya UDASA iliyotolewa jana tarehe 23 Oktoba.

Katika tamko lake, Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye, ameleza kuwa chuo hicho kwa namna yoyote ile, hakihusiki na tamko la UDASA.

Amesema, “UDASA ni Jumuiya ya Wanataaluma, yenye uongozi wake, katiba yake na misimamo yake ya kisomi.

Hakuna pahala popote ambapo tamko letu limetaja au kuhusisha na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Kilichosemwa si msimamo wa UDSM wala viongozi wake ambao nao ni wanachama wa UDASA. Tamko la UDASA ambalo limesainiwa na mwenyekiti wake, Prof. Dk. Ichumbaki ndiyo msimamo wa Jumuiya ya Wanataaluma wa UDSM,” imeeleza taarifa hiyo.

Imeongeza, “Uongozi wa UDASA utawachukulia hatua za kinidhamu wana-UDASA wote ambao watakiuka matakwa ya kikatiba ya UDASA na kukataa kuwa sehemu ya kutekeleza jukumu hili muhimu, yaani uwajibikaji wa kijamii wa wasomi.”

About The Author

error: Content is protected !!