Tundu Lissu akiwa mahakamani
WAKATI Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akidai kuwa kesi ya uhaini dhidi yake imefunguliwa kwa ajili ya uchaguzi. Serikali imekanusha madai hayo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Lissu anayshtakiwa kwenye Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam kwa shauri Na. 19605/2025 linalosikilizwa na jopo la majaji watatu liliongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, masjala ndogo ya Iringa Jaji Dunstan Ndunguru akishirikiana na Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde., amedai kuwa ashikiliwa kwa ajili ya uchaguzi
Jana tarehe 22 Oktoba, wakati shauri hilo limeahirishwa Lissu alieleza kuwa anaendelea kusalia gerezani kwa sababu ya uchaguzi “Kuanzia sasa ninakaa gerezani kwa sababu ya tarehe 29 tu (ndio siku ya uchaguzi) kesi imekwishaaa.”
Leo tarehe 23 Oktoba 2025, Wakili wa Serikali Renatus Mkude akijibu hoja za Lissu kuhusu ahirisho la kesi hiyo sambamba na hoja ya dhamana ya Lissu alida kuwa kuwa kesi hiyo haijafunguliwa kwa ajili ya uchaguzi .
“Swala la uchaguzi unaotarajia kufanyika nchini hauna uhusiano na chochote mpaka tunafungua mashtaka haya tumefuata utaratibu na uchaguzi hauhusiani kabisa,” alidai Wakili Mkude.
Mkude amedai mahakamani hapo kuwa upande wa mashtaka utakwenda na shauri hilo mpaka mwisho mahakama ndio itakayoamua.
“Upande wa mashtaka umefungua mashtaka na tumefuata utaratibu na kwasasa kesi inasikilizwa upande wa mashtaka na tunajua tuna ushahidi na kusema kwamba hakuna ushahidi wa kuleta mahakamani huo ni upande wa mashtaka na tunajua tuna ushahidi gani na upande wa mashtaka hatujafunga.
“Upande wa mashtaka una mashahidi 30 na sisi tunajua tuna ushahidi gani na tutakapo funga ushahidi Mahakama itatoa hukumu kwamba mshatakiwa ana kesi ya kujibu au la,” amedai Wakili Mkude.
ZINAZOFANANA
Chadema yataka Heche achiwe huru
Hatuna mawakala, kura zitalindwa na INEC
UDASA yageuka mbogo, yauvaa uongozi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam