Peter Kibatala
MAWAKILI wa Balozi Mstaafu Humphrey Polepole wametoa taarifa kwa umma wakizitaka mamlaka za usalama nchini kutumia rasilimali na mbinu zote kuhakikisha usalama wake na kutoa taarifa kwa Watanzania na dunia nzima. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Katika taarifa iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala, imeelezwa kuwa Polepole amehudumia taifa kwa muda mrefu katika nafasi mbalimbali za utumishi wa umma, hivyo ana haki ya kulindwa kisheria na kiusalama kama raia.
Aidha, mawakili hao wamesisitiza kuwa wataendelea kutoa taarifa zaidi kuhusu maendeleo ya jambo hili, zikiwemo hatua wanazochukua kwa kushirikiana na watu na taasisi mbalimbali duniani kote.
Tamko hilo limekuja kufuatia taarifa zinazodai kutekwa kwa Polepole usiku wa kuamkia tarehe 6 Oktoba 2025, tukio lililosababisha taharuki kubwa kwa wananchi.
ZINAZOFANANA
Wazili Mkuu kuongoza mazishi ya Kitaifa ya Lukuvi Idodi Iringa
Lukuvi atakumbukwa kama nguzo muhimu wa familia
Meridianbet yaweka alama muhimu kwa kuwakumbuka wagonjwa waliolazwa