September 6, 2025

Mwanahalisi Online

Habari za Uhakika

Chadema yalaani tukio la kushambuliwa mwandishi EATV

Marco Kilo

 

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelaani kitendo cha Mwandishi wa Televisheni ya EATV, Marco Kilo kushambuliwa na maofisa wa Kampuni ya mabasi ya mwendokasi (UDART). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Tarifa ya Brenda Rupia, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho ya leo tarehe 6 Septemba 2025, imesema kuwa chama hicho kinatoa wito kwa jeshi la Polisi kuchukua hatua ya haraka za kisheria dhidi ya maofisa UDART waliohusika kumsambulia Kilo, tarehe 4 Septemba 2025.

“Chadema tunatoa wito kwa Jeshi kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka za kisheria dhidi ya maofisa wa UDART waliohusika katika tukio hilo,” imeeleza taarifa ya Rupia.

Rupia ametoa wito kwa vyombo vya habari, taasisi za haki za binadamu kuhakikisha mwandishi Kilo anapata haki yake.

About The Author

error: Content is protected !!