
MGOMBEA urais, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu ujao, Samia Suluhu Hassan, ameendelea kujimwagia sifa ya kutekeleza ahadi zake. Anaripoti Zakia Nanga, Dar es Salaam … (endelea).
Akizungumza na maelfu ya wananchi mjini Njombe jana, Samia alikumbusha utekekezaji wa baadhi ya yale aliyoahidi.
Alisema, mwaka 2022 alizindua hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Njombe na kusisitiza kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, serikali imefanikisha maboresho ya hospitali saba za wilaya.
Alisema, serikali imeongeza vituo vya afya kumi na tatu na kuhakikisha huduma za afya zinapatikana karibu na wananchi bila kulazimika kusafiri umbali mrefu.
Aidha, Rais Samia alikumbusha ahadi yake ya kuanzisha tawi la chuo kikuu mkoani humo, akieleza kuwa ujenzi wa chuo hicho, unaendelea vizuri.
“Chuo kikuu hicho kimekusudiwa kutoa mafunzo katika fani za ufugaji, kilimo, mawasiliano na teknolojia, hatua itakayowawezesha vijana wa Njombe kupata ujuzi na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya mkoa na taifa kwa ujumla,” alieleza.
Rais Samia yuko katika ziara ya kampeni itakayomuwezesha kushinda uchaguzi mkuu wa Oktoba na hatimaye kuunda serikali.
Hata hivyo, kampeni za mwaka huu, zinaonekana kudoda kufuatia hatua ya chama kikuu cha upinzani nchini – Chama cha Demokrasia na Maendeleo – kutoshiriki uchaguzi huo.
Chadema kimeamua kutoshiriki uchaguzi huo, baada ya chama tawala, kugoma kuandika Katiba mpya na kufanyiwa marekebisho kwa sheria za uchaguzi.
ZINAZOFANANA
Askofu Mwanamapinduzi akimbia nchini akidai kusakwa kuuwawa
Chadema yalaani tukio la kushambuliwa mwandishi EATV
Rais Mwinyi akemea kauli za uchochezi